Tunaunda zana na mazingira ya kujifunza kupitia mchezo kwenye blockchain ya Cardano.
Tushirikiane kujenga mifumo ya elimu ya siku zijazo – ili kuwezesha upatikanaji wa elimu kwa kila mtu.
Stay up to date and subscribe to our newsletter.
Lugha
Kujifunza
Mchezo
Mradi wetu wa kwanza ni mchezo wa wachezaji wengi mtandaoni kwa ajili ya kujifunza lugha, ushirikiano na kubadilishana uzoefu.
SANDBOX-MMO
MMO ni michezo ya kompyuta inayowezesha mamia ya maelfu ya wachezaji kucheza kwa wakati mmoja kwenye ulimwengu mmoja unaoendelea kupitia mtandao. Wachezaji kwa kawaida hutangamana na kuwasiliana wao kwa wao na kuunda maendeleo ya mchezo pamoja. Katika mchezo wetu, kila lugha ina ulimwengu wake, unaokaliwa na kutengenezwa na jamii yake. Wazungumzaji wa L1 iliyothibitishwa (L1 = lugha ya kwanza) na wachezaji wa kiwango cha juu toka kwenye DAO ( Shirika lenye Uhuru wa Madaraka ) ili kutawala kidemokrasia ulimwengu wao.
KUJIFUNZA KWA MSINGI WA MCHEZO
Mchezo umeundwa kwa ajili ya kujifunza kwa vitendo katika mazingira ya kijamii, salama na yanayoongozwa ya 3D.
Tunafungua majaribio na uchunguzi kama njia zinazofaa za kujifunza kwa kujitegemea. Unaweza chunguza vipengele vyote vya mazingira yako ili kujifunza msamiati mpya na kugundua maelezo zaidi.
Makosa yanaonekana tu kama majaribio, sio kushindwa, na hutoa fursa ya kuboresha. Unaweza rudia kazi zote mara nyingi upendavyo, na uchukue muda mwingi kadiri unavyohitaji ili kuyamudu. Utapatiwa msaada na mrejesho wa mara moja ili kukuongoza vyema kwenye safari yako yakubobea katika lugha uliyochagua kujifunza.
JAMII
Shirikisha uzoefu wako binafsi wa kujifunza watu wengine kutoka duniani kote. Fanya miunganisho ya kijamii, kitamaduni au mipaka ya kitaifa. Wasiliana, fanya mazoezi, na kucheza katika mazingira anuwai na ya kukaribisha ambayo hukua katika ugumu na uzoefu wako na sifa.
THAMANI
Mchezo ni bure 100% na unalipa wachezaji. Vyanzo vyote vya mapato vya mchezo hubadilishwa kwa
ADA (tokeni ya Cardano) na kusambazwa tena kwenye hazina ya mchezo ambayo huongeza thamani ya sarafu ya ndani ya mchezo ( Tokeni yetu wenyewe ).
Michango na ushiriki unaofaa hutuzwa tokeni na zawadi maalum/NFTs. Kwakuongezea, DAO ya kila ulimwengu hutoa Hati-tambulishi Iliyothibitishwa (VCs) ya DID za watumiaji ( Vitambulisho Zilizogatuliwa) kupitia Atala PRISM, ambayo ni suluhisho la SSI la Cardano. Hii inaruhusu washiriki kuthibitisha maendeleo yao na kusimama ndani ya mchezo na nje.
JUMUIYA
Maudhui na thamani yote katika mchezo huundwa kwa pamoja na kusimamiwa na jumuiya.
Educhainment huunda tu zana za kuunda mchezo kwa njia iliyogatuliwa na inayojumuisha wote.
Tunajitahidi kusaidia watumiaji wote kadri iwezekanavyo kupitia wahariri angavu na miongozo/mazoea bora, na kuwawezesha.
UUMBAJI SHIRIKISHI
Kila mtu anaweza kuchangia kwenye mchezo kwa njia yake mwenyewe na kwa kiwanga anacho chagua. Fanya kile wewe unachopenda zaidi au jaribu vitu vipya. Kwa mfano, kuwa mbunifu, mkalimani, msimamizi, mwalimu au mwandishi kwa viwango na ulimwengu!
Tusaidie kwa pamoja kujenga mifumo ya elimu ya siku zijazo!
SETI YA LUGHA ZA KUANZIA
Lengo letu ni kuruhusu watu wengi iwezekanavyo kufikia jukwaa letu na kuhusika katika mchakato wa kuliunda. Ndiyo maana tunazingatia lugha zinazozungumzwa zaidi kwanza, na kisha kuongeza zile ambazo tunafikiri ni muhimu sana kwa mfumo ikolojia wa Cardano.
Lugha Zinazozungumzwa Zaidi:
Takriban nusu ya idadi ya watu duniani huzungumza mojawapo ya lugha rasmi za Umoja wa Mataifa.
-
Kiarabu Sanifu
Kichina cha Kawaida
-
Kiingereza
-
Kifaransa
-
Kirusi
-
Kihispania
Lugha zilizopewa kipaumbele:
Kiamhari na Oromo
Ethiopia ni moja wapo ya wafuasi wa awali wa Cardano katika sekta ya elimu. Zaidi ya 60% ya watu wake huzungumza Kiamhari au Kioromo.
Kijapani
Cardano ina uhusiano wa kihistoria na Japan. Kwa mfumo wake mzuri wa ikolojia na uorodheshaji wa hivi majuzi wa ADA katika masoko yao ya fedha, inatoa uwezekano mkubwa wa kupitishwa kwa blockchain.
Kiswahili
Kiswahili ni lugha muhimu katika nchi nyingi za Kiafrika, na hutoa fursa za kibiashara na njia ya mawasiliano.
Lugha lengwa zinazofuata:
Kibengali, Kiurdu, Kitamil, Kihausa, Kiajemi, Kituruki, Kiebrania, Kigeorgia, ... Kwa muda mrefu, tunataka kutoa nafasi kwa kila utamaduni wa lugha, fursa ya kujenga ulimwengu wake na kuwa mojawapo ya lugha zinazotumika.
Team >
MAALUM
SHUKRANI
KWA
wanachama wa zamani
Nora Schumann
na
Ben Jesus Kneiphof